Entertainment

DRAKE ANG’AA KWENYE TUZO ZA BILLBOARD MUSIC AWARDS 2022

DRAKE ANG’AA KWENYE TUZO ZA BILLBOARD MUSIC AWARDS 2022

Rapa Drake ameendelea kung’aa kwenye Tuzo za Billboard (Billboard Music Awards) ambapo usiku wa kuamkia leo ametengeneza rekodi ya kuwa msanii aliyeshinda Tuzo nyingi zaidi, akishinda Jumla ya Tuzo 34 kwenye historia ya BBMA’s.

Drizzy ameshinda Tuzo ya Top Rap Artist, Top Rap Album kupitia album yake ya Certified Lover Boy na Top Artist.

Kwa upande wa muziki wa Injili Rapa Kanye West ametamba kwa kushinda Tuzo Tatu; Top Christian Album kupitia album yake ya DONDA, Top Christian Artist na Top Gospel Artist.

Wasanii wengine walioshinda tuzo za billboard ni pamoja na Olivia Rodrigo ambaye alishinda Tuzo ya Msanii Bora Chipukizi huku Justin Bieber akishinda tuzo ya Top Collaboration kupitia ngoma ya STAY aliyomshirikisha The Kid Laroi .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *