
Rapa kutoka Marekani Drake ameripotiwa kutia saini dili nono na Universal Music Group ambalo linadaiwa kuwa na thamani ya dola milioni 400 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 46 za Kenya .
Habari hiyo imethibitishwa kupitia simu ya mapato ya UMG (Q1 earnings call), licha ya kuwa kiasi halisi hakikuwekwa wazi lakini wadadisi wa mambo wametaja kuwa ni kiasi cha pesa kisichopungua dola milioni 400, ingawa kinaweza kuwa kikubwa zaidi hicho.
Hapo awali Drake aliwahi kusaini dili na Cash Money kupitia ‘Republic Records, inazomilikiwa na Universal Music Group, na amesaini tena na UMG mkataba mpya, ambao makubaliano yatahusisha kurekodi, kusambaza kazi za muziki, bidhaa za mavazi pamoja na miradi mingine.
Kwa mujibu wa wakili mmoja katika tasnia ya muziki nchini Marekani, “Drake ana uwezo wa kujadiliana ili kufikia muafaka wa mgawanyiko wa faida kamili