
Rapa maarufu Drake ameonesha tena kiwango chake cha juu cha ukarimu na ushawishi kwenye muziki baada ya kukodi ndege binafsi (Private Jet) yenye thamani ya Dola Milioni 80, kwa ajili ya kuwachukua Bloggers, Waandishi wa Habari na Streamers maalum kwenda jijini London kuhudhuria tamasha kubwa la Wireless Festival.
Drake, ambaye ndiye mtumbuizaji mkuu (Headliner) wa tamasha hilo, ameandaa safari hiyo kama sehemu ya kuwatambua na kuwahusisha watu muhimu katika tasnia ya burudani na mitandao ya kijamii nchini Marekani. Tamasha hilo litafanyika kwa siku tatu kuanzia leo Julai 11 hadi Julai 13, likitarajiwa kuvutia maelfu ya mashabiki kutoka sehemu mbalimbali za dunia.
Hatua hii inaonyesha namna Drake anavyothamini vyombo vya habari na majukwaa ya kidijitali katika kuendeleza na kusambaza muziki wake kimataifa.