Msanii mkongwe, Dudu Baya, ameibua tuhuma nyingine nzito dhidi ya Mdau wa Burudani, Mwijaku, kwa kusema kuwa alifutwa kazi na kituo cha Clouds TV kwa wizi wa simu ya mfanyakazi mwenzao.
Kwa mujibu wa Dudu Baya, tukio hilo lilitokea kipindi ambacho Mwijaku alikuwa mwigizaji katika moja ya vipindi vilivyokuwa vinarushwa na runinga hiyo. Anadai kuwa baada ya simu hiyo kupotea, ilipatikana katika mji wa Morogoro ikiwa mikononi mwa mdogo wa Mwijaku, hali iliyozua mashaka makubwa ndani ya uongozi wa kituo hicho.
Dudu Baya anasema kuwa kufuatia sakata hilo, uongozi wa Clouds TV wakati huo, ukiongozwa na aliyekuwa bosi marehemu Ruge Mutahaba, ulichukua hatua kali dhidi ya Mwijaku. Anadai kuwa Ruge alimfuta kazi na kumwonya asiwahi tena kumwona kwenye kituo hicho.
Aidha, Dudu Baya ameonesha kushangazwa na hatua ya Mwijaku kutumia jina la marehemu Ruge Mutahaba mara kwa mara kwenye masuala yake ya kutafuta kiki mtandaoni ilhali alifukuzwa kazi kwa fedheha kubwa.
Kauli ya Dudu Baya imekuja baada ya Mwijaku kudai kuwa hana makazi na hivyo amehamia kwenye maeneo ya burudani kupoteza muda ambapo alienda mbali na kujigamba kuwa anamiliki TV ya inchi 100, magari na majengo ya kifahari.