Tech news

Google Yaunganisha Akili Bandia ya Gemini Ndani ya Gmail

Google Yaunganisha Akili Bandia ya Gemini Ndani ya Gmail

Google imetangaza rasmi kuingiza akili bandia yake ijulikanayo kama Gemini ndani ya mfumo wa barua pepe wa Gmail, hatua inayokuja na mabadiliko makubwa kwa watumiaji wake duniani kote.

Kuanzia sasa, watumiaji wa Gmail wataanza kuona mwonekano mpya wa Gmail, sambamba na huduma mpya za akili bandia zitakazosaidia kuandika na kujibu barua pepe kwa urahisi zaidi.

Kwa mujibu wa Google, mfumo huu wa Gemini utaweza kusoma na kuchambua barua pepe za mtumiaji, kutambua mtindo na tone la uandishi, kisha kusaidia kuandika barua pepe zinazoendana na style ya mtumiaji husika.

Mabadiliko haya yanatarajiwa kutekelezwa kwa watumiaji wote wa Gmail, ikiwa ni sehemu ya mpango wa Google wa kupanua matumizi ya AI katika huduma zake za kila siku.

Hata hivyo, hatua hiyo imeibua wasiwasi kutoka kwa baadhi ya watumiaji, wakieleza hofu juu ya masuala ya faragha. Baadhi yao wanasema hawajisikii salama kufahamu kuwa barua pepe zao binafsi zinaweza kusomwa na mfumo wa akili bandia wa Google.

Licha ya malalamiko hayo, Google imesisitiza kuwa inalinda faragha ya watumiaji wake na kwamba matumizi ya AI yanafanyika kwa kuzingatia sera za usalama na faragha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *