
Mwanamuziki wa Dancehall Dufla Diligon amelitaja jina la EP yake mpya anayotarajia kuiachia hivi karibuni.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema EP hiyo ameiita “Zone”, na ana mpango wa kuachia wimbo wa kwanza kutoka kwa EP hiyo ambayo ameitaja kuwa ni bonus track.
“Mheshimiwa @jalangoo alilalamika sana kwamba sijatoa ngoma siku nyingi. This week we drop a bonus track off my incoming EP ‘ZONE’ Thank you to everyone who keep supporting me. Much love to you all 💪🏿❤️🙏🏿”, Aliandika.
Hata hivyo, Dufla ambaye amekuwa akisuasua kimuziki bado hajaweka wazi ni lini EP hiyo itatoka rasmi na itakuwa na nyimbo ngapi.
Ikumbukwe kuwa, huu unaenda kuwa ujio wa kwanza kwa Dufla Diligon kuachia tangu ajiondoe kwenye label ya muziki ya GrandPa records.