Entertainment

Dyana Cods Atangaza Ujio wa Albamu Yake Mpya “Ghetto Story”

Dyana Cods Atangaza Ujio wa Albamu Yake Mpya “Ghetto Story”

Hitmaker wa ngoma ya “Set It”, Msanii Dyana Cods, ametangaza ujio wa albamu yake ya nne kwa jina Ghetto Story, hatua iliyowaacha mashabiki wake na hamu kubwa ya kusikia kazi hiyo mpya.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram, Dyana alipakia mfululizo wa picha za kisanii na kusindikiza kwa maneno mafupi yenye uzito yaliyosomeka “#GhettoStory 4th album coming soon.”

Ingawa mrembo huyo hakuweka wazi tarehe rasmi ya kuachia albamu hiyo, ujumbe huo umeibua mjadala na matarajio makubwa kutoka kwa mashabiki na wadau wa muziki, wengi wakitarajia kazi iliyojaa maudhui ya maisha halisi na uhalisia wa mitaani kama jina la albamu linavyoashiria.

Albamu hii inatarajiwa kuwa mwendelezo wa mafanikio ya Dyana Cods katika muziki wa Kenya, huku wengi wakisubiri kuona ushirikiano mpya, ujumbe mzito, na ladha mpya ya kipekee inayotambulika kwa mtindo wake.

Ikumbukwe kwamba Dyana Cods tayari ameachia albamu tatu tangu aanze safari yake ya muziki, ambazo ni THANK ME LATER (2022), River Lake Nilote (2023), na Rong Manners (2024).