Entertainment

Dyana Cods Atetea Wasanii Kuhusu Malipo Kutoka Serikalini

Dyana Cods Atetea Wasanii Kuhusu Malipo Kutoka Serikalini

Mwanamuziki wa Kenya, Dyana Cods, amejibu lawama zinazowakumba wasanii wanaofanya maonyesho kwenye hafla za serikali na kulipwa kwa kazi zao. Kundi la wakosoaji limekuwa likidai kwamba hatua ya wasanii kushiriki katika hafla hizo ni sawa na kuunga mkono serikali ya Rais William Ruto, hali ambayo imewafanya baadhi ya wananchi kuwataka wasanii wasipokee malipo hayo.

Kwa mujibu wa Dyana Cods, mtazamo huo ni wa kupotosha kwani sanaa ni taaluma kama nyingine, na msanii anayelipwa na serikali hastahili kuhusishwa moja kwa moja na masuala ya kisiasa.

Hitmaker huyo wa Set It, amesisitiza kuwa walimu, madaktari na kazi nyingine pia hulipwa na serikali bila kulaumiwa, hivyo ni upotoshaji kuona malipo ya wasanii yakigeuzwa kuwa ajenda ya kisiasa.

Aidha, amesema wasanii wanachangia pakubwa katika burudani, kukuza utamaduni na kuimarisha taswira ya taifa, hivyo hawapaswi kubezwa wala kuhusishwa moja kwa moja na siasa kwa sababu ya kazi yao.

Kauli yake imekuja wakati ambapo kumekuwa na maoni tofauti kuhusu nafasi ya wasanii kwenye hafla za kitaifa. Wapo wanaoamini kuwa fedha za umma zinapaswa kuelekezwa zaidi kwenye sekta za kijamii, huku wengine wakisisitiza kuwa wasanii pia ni wataalamu wanaostahili kulipwa kwa kazi zao kama walivyo wataalamu wengine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *