Entertainment

ED SHEERAN AKOSHWA NA WIMBO WA PERU WAKE FIREBOY DML

ED SHEERAN AKOSHWA NA WIMBO WA PERU WAKE FIREBOY DML

Mwimbaji hodari wa nchini Uingereza Ed Sheeran amezimika na dundo la Fireboy DML ‘Peru’ hivyo ameamua kufanya Remix ya wimbo huo.

Kwenye mahojiano na Elton John, Ed Sheeran amesema mkali huyo kitoka nchini Nigeria alimtafuta kupitia mtu mwingine na kuomba aibariki ngoma hiyo.

Baada ya kuisikiliza, Ed Sheeran anakiri kwamba ilimuingia na kumtengenezea uraibu (addiction) kiasi cha kuingia studio na kufanya Remix.

Ed Sheeran ni shabiki wa muziki wa Afrika, mwaka 2017 alifanya ngoma iitwayo ‘Bibia Be Ye Ye’ ambayo video yake ilifanyikia nchini Ghana na kuonesha mandhari ya taifa hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *