Entertainment

Eddy Kenzo aandika historia Afrika Mashariki, Atajwa kuwania tuzo za Grammy.

Eddy Kenzo aandika historia Afrika Mashariki, Atajwa kuwania tuzo za Grammy.

Mwanamuziki wa nchini Uganda Eddy Kenzo ametajwa kuwania Tuzo za Grammy mwaka 2023 ambapo ametajwa katika kipengele cha Best Global Music Performance na wimbo wake ‘Gimme Love’ aliomshirikisha Matt B.

Eddy Kenzo anakuwa msanii wa kwanza kutoka ukanda wa Afrika Mashariki kutajwa kuwania Tuzo hizo kubwa na maarufu duniani. Aliwahi pia kuwa msanii pekee aliyeshinda Tuzo ya BET kwa Afrika Mashariki kabla ya Rayvanny kuinyakua pia mwaka 2017.

Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa Februari 05, mwaka 2023.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *