
Hitmaker wa “Nsimbudde”, Msanii Eddy Kenzo ametoa changamoto kwa serikali ya Uganda kuwawezesha wasanii wa ndani kifedha ili waweze kurekodi nyimbo za kizalendo.
Kwenye mahojiano na Tawfiq Media Ug Kenzo amesema wasanii wengi wanaogopa kuachia nyimbo za kizalendo kwa sababu aina hiyo ya muziki haina soko.
Mshindi huyo wa BET amesisitiza kuwa wasanii wengi wanafanya muziki kama biashara na ndio maana wengi wao wanawekeza kwenye muziki ambao unawaingizia kipato.
Kauli ya Eddy Kenzo imekuja mara baada ya kuulizwa mbona wasanii wengi nchini Uganda hawatoi nyimbo za kizalendo katika miaka ya hivi karibuni.