Gossip

Eddy Kenzo Atetea Hadhi Yake ya Kimataifa Baada ya Kukejeliwa na Bebe Cool

Eddy Kenzo Atetea Hadhi Yake ya Kimataifa Baada ya Kukejeliwa na Bebe Cool

Msanii maarufu wa Uganda na mshindi wa tuzo za kimataifa, Eddy Kenzo, amemjibu vikali Bebe Cool kufuatia kauli yake aliyodai kuwa hakuna msanii wa kiwango cha kimataifa nchini Uganda kwa sasa akiwemo Kenzo mwenyewe.

Katika mahojiano yake na kituo kimoja cha runinga, Kenzo ameeleza kuwa hana haja ya kuthibitisha thamani yake kwa mtu yeyote, kwani mafanikio yake yanajieleza yenyewe. Amemtaja Bebe Cool kama mbinafsi asiye na uelewa wa hali halisi ya soko la muziki duniani.

Kauli ya Kenzo imekuja mara baada ya Bebe Cool kudai katika mahojiano na mtangazaji Kasuku kwamba Eddy Kenzo hajafikia kiwango cha kuwa msanii wa kimataifa, licha ya kuwa na tuzo na kutambulika Afrika.

Mvutano huu umeibua mjadala mkubwa mitandaoni, huku mashabiki wa pande zote mbili wakitupiana maneno. Wengi wanamtetea Kenzo kama nembo ya muziki wa Uganda duniani, huku wengine wakisema Bebe Cool anaangalia mafanikio ya kimataifa kwa mizani tofauti.

Hii si mara ya kwanza wawili hao kutofautiana. Mnamo mwezi Juni mwaka huu, walitupiana maneno makali kuhusu tamasha la Diamond Platnumz lililofanyika huko Ntungamo, kila mmoja akionesha msimamo tofauti.