
Mwanamuziki Edrisa Musuuza maarufu Eddy Kenzo amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu madai ya kumtwanga shabiki na kipaza sauti kwenye moja onesho lake juzi kati.
Akizungumza kuhusu tukio hilo Eddy Kenzo amesema hakufurahishwa na kitendo cha shabiki kumwagia pombe akiwa jukwaani jambo ambalo lilimkasirisha na akajipata amemrushia kapaza sauti kwani kinywaji hicho kilikuwa kinatoa harufu mbaya.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Nsimbudde” ametejitea namna ambavyo alichukulia tukio hilo kwa kusema kwamba hapendi kabisa kuvunjiwa heshima kwa kuwa yeye ni moja kati ya watu ambao wanapenda sana amani.
Utamkumuka Septemba mwaka wa 2014 Kenzo alimshushia kichapo cha mbwa mtangazaji wa Dembe FM Isaac Katende maarufu kama Kasuku kwenye mkao na wanahabari huko Centenary Park kwa madai ya kumzungumzia vibaya.