Entertainment

EDDY KENZO AWALAUMU WASANII WAKONGWE KWA KUIGAWANYA TASNIA YA MUZIKI UGANDA

EDDY KENZO AWALAUMU WASANII WAKONGWE KWA KUIGAWANYA TASNIA YA MUZIKI UGANDA

Mwanamuziki Eddy Kenzo amewalaumu wasanii wakongwe kwa migawanyiko inayohushudiwa kwa sasa kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda.
Mwimbaji huyo ambaye ni mshindi wa Tuzo ya BET mwaka wa 2015 anaamini wanamuziki wakongwe wameshindwa kuwaleta wasanii pamoja jambo ambalo limepelekea wasanii wa kizazi kipya kujigawa kwenye makundi mbali mbali.

Lakini pia amesema viongozi wa Chama cha Wanamuziki wa Uganda (UMA) hawana budi kuweka kando maslahi yao binafsi na kufanya kazi kuelekea ustawi wa wanamuziki wote.

“Nina tatizo na chama, nadhani hakiko kwenye njia sahihi. Imezua mgawanyiko miongoni mwa wanamuziki katika tasnia hii. Viongozi lazima wazingatie kufanya kazi kwa manufaa ya wanamuziki wote,” aeleza.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Nsimbudde” amethibitisha kuwa hatashiriki katika uchaguzi ujao wa UMA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *