
Mwanamuziki wa nyimbo za injili nchini Eko Dydda ametia nia ya kugombea uwakilishi wadi ya Mathare Kaskazini kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.
Kupitia ukurasa wake wa instagram hitmaker huyo wa “Niko na Reason” amesema kuwa amesukumwa kugombea kiti cha uwakilishi wadi wa eneo hilo kutokana na kero ambazo vijana wamekutana nazo kwenye suala la kusaka ajira.
Aidha amesema ni muda wa vijana kuwania nyadhafi za uongozi kwani viongozi waliochaguliwa wamefeli kutekeleza ahadi walizozitoa kwa wananchi.
Hata hivyo ametoa changamoto kwa vijana kujisajili kama wapiga kura ili waweze kuleta mabadiliko katika maeneo ambayo wanatoka kwa kuwachagua viongozi wawajibikaji kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Eko dydda ni moja kati ya wasanii ambao wamekuwa wakishinikiza kumaliza ukabili miongoni mwa wakenya kwani mwaka wa 2015 aliacha kutumia jina la ukoo wake na akaanza kutumia Eko Dydda kama jina lake rasmi.