
Baadhi ya wafuasi wa mitandao ya kijamii nchini wamemjia juu mchekeshaji Eric Omondi baada ya kushare Video akicheza wimbo mpya wa Diamond Platnumz uitwao “Chitaki”
Wakenya kwenye uwanja wa comment wamemshambulia vikali mchekeshaji huyo na kumuita mnafiki kwa kitendo cha kuupigia upata muziki wa kigeni katika mambo yake mitandaoni ilhali amekuwa mstari wa mbele kupinga muziki huo kupigwa kwenye vyombo vya habari nchini
Omondi kwa muda mrefu amekuwa akilaumu vyombo vya habari nchini na Wakenya kwa ujumla akidai kuwa wameukimbia muziki wao na kukumbatia muziki kutoka nje haswa Tanzania na Nigeria.