
Mchekeshaji maarufu nchini Eric Omond omeonekana kutofurahishwa na kitendo cha Omah Lay kutofanya kazi na mpenzi wake Tanasha Donna licha ya ukaribu wao.
Katika mahojiano yake na Plug TV Omondi amesema kitendo cha Omah Lay kufanya kolabo na Justin Bieber inaonyesha ni jinsi gani hitmaker huyo wa “Godly” hana mpango wa kuupeleka muziki wa Tanasha Donna kimataifa.
Utakumbuka kwa muda sasa Omah Lay amedai kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Tanasha Donna ila wawili hao wamekuwa wakikanusha madai hayo kwa kusema kwamba uhusiano wao ni wa kirafiki tu