Entertainment

Eric Omondi awakosoa wasanii wa Kenya kwa kushindwa kutangaza kazi zao mitandaoni

Eric Omondi awakosoa wasanii wa Kenya kwa kushindwa kutangaza kazi zao mitandaoni

Mchekeshaji maarufu nchini Eric Omondi anazidi kulia na uwekezaji unaofanywa n awasanii wa Kenya na wasanii wa Tanzania huku akitolea Mfano Wasanii wawili waliotoa burudani kwenye tamasha la Sol Fest ambao ni Harmonize na Nadia Mukami.

Omondi amesema kuwa msanii Harmonize ametumia muda wake kuandaa timu ambayo ameibeba kutoka Tanzania mpaka Nairobi akiwemo mpiga picha ambapo ameweka video Tatu zikionesha matukio yote ya utumbuizaji wake kwenye tamasha hilo ambapo baadhi mashabiki zake wanadhani Show hiyo iliandaliwa na Harmonize pekee na kuudhuriwa na watu 15,000.

Mbali na hilo Eric Omondi ametolea Mfano Msanii kutoka Nchini Kenya Nadia ambaye anadai ni miongoni mwa wasanii waliotumbuiza vizuri zaidi kwenye tamasha la Sol Fest lakini kwenye mitandao yake ya kijamii ameweka picha akiwa kwenye ukuta usio eleweka kitu ambacho kimefanya mashabiki zake kushindwa kuelewa kama alitumbiza katika show hiyo.

Hata hivyo amewataka wasanii wa Kenya kuwekeza kwenye suala la branding katika mitandao ya kijamii ili kuleta taswira nzuri kwa mashabiki zao walio nje ya nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *