Entertainment

Eric Omondi awaonya mapromota dhidi ya kuwaleta wasanii wa kigeni

Eric Omondi awaonya mapromota dhidi ya kuwaleta wasanii wa kigeni

Mchekeshaji Eric Omondi amewaonya mapromota wa muziki dhidi ya kuwaleta wasanii wa kigeni  kutumbuiza nchini Kenya.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Omondi ameapa kupambana na promota  atakayekwenda kinyume na agizo lake kwa kuhakikisha tamasha lake la muziki linasambaratika.

Aidha mchekeshaji huyo amesitikishwa na kitendo cha mapromota kujihusisha visa vya kuwatapeli wasanii wa mataifa mengi, jambo ambalo amedai huenda ikachafua taswira ya taifa la kenya kwenye jamii ya kimataifa.

“This is MY ORDER to all PROMOTERS in this Country!!! DO NOT!!! and I repeat DO NOT invite anymore Foreign Artists until we have Order. First of all you are killing our own and then secondly you are shaming us Abroad!! DO NOT!!! And if you Try I’ll ensure your EVENT FLOPS!!! TRY ME IDIOTS😡😡😡😡 TRY ME!!!”, Ameandika.

Kauli ya Eric Omondi imekuja mara baada ya msanii wa Amapiano kutoka Afrika kusini DJ Chichi kukwama nchini kwa kipindi cha mwezi mmoja kufuatia hatua ya promota aliyempa mwaaliko kushindwa kugharamia mahitaji yake ya msingi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *