Sports news

Esperance Yaipa Flamengo Tiketi ya Mapema, Yaweka Presha Kwa Chelsea

Esperance Yaipa Flamengo Tiketi ya Mapema, Yaweka Presha Kwa Chelsea

Klabu ya Esperance Tunis kutoka Tunisia imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Los Angeles FC ya Marekani katika mchezo wa Kundi D wa Kombe la Dunia la FIFA ngazi ya klabu, na hivyo kuweka matumaini ya kufuzu hatua ya 16 bora.

Bao pekee la mchezo huo lilifungwa na Belaili dakika ya 71, ambalo lilitosha kuipa timu hiyo Tunis nafasi ya tatu katika msimamo wa kundi.

Ushindi huu umewafanya vinara wa Kundi D, Flamengo ya Brazil, kuwa timu ya kwanza rasmi kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Dunia la Klabu mwaka 2025.

Mchezo wa mwisho wa Kundi D utakuwa kati ya Esperance Tunis na Chelsea, ambapo matokeo ya mchezo huo yataamua ni timu gani itakayoungana na Flamengo kwenye hatua ya 16 bora. Chelsea inahitaji hata sare ili kukata tiketi ya kufuzu, huku Esperance ikihitaji ushindi pekee ili kusonga mbele katika michuano hiyo