Meneja wa msanii Breeder LW, Eugene Baron, ameamua kumpa rapa huyo maua yake akiwa bado hai kwa kumtaja kama Mfalme wa New Age Rap nchini Kenya.
Kupitia ujumbe aliouchapisha mtandaoni, Baron amesema hakuna msanii anayeweza kulinganisha ujuzi na uwezo wa Breeder LW katika muziki wa kizazi kipya.
Amesema kuwa Breeder LW amefikisha muziki wa rap katika kiwango cha juu kisichoweza kufikiwa kirahisi, hata na wasanii kutoka nchi jirani. Ameongeza kuwa hata baadhi ya wasanii wa Tanzania wanatambua uwezo huo na wanaheshimu ubunifu wa Breeder.
Kauli hiyo imepokelewa vyema na mashabiki wengi, ambao wamesifu hatua ya meneja huyo kutambua juhudi za msanii wake mapema badala ya kusubiri mafanikio au misiba.