
Mwiigizaji maarufu kutoka Marekani Karrueche Tran amepuzilia mbali uvumi wa muda mrefu kuwa anatoka kimapenzi na rapa Quavo wa kundi la Migos.
Akiwa Mbele ya kamera za TMZ, Karrueche amekanusha madai hayo kwa kusema kwamba uhusiano wake na rapa huyo ni wa kirafiki tu na kwa sasa anafurahia maisha yake akiwa hana mpenzi yaani single!
Uvumi wa Karrueche Tran kutoka kimapenzi na Quavo ulianza tangu mwaka 2017 baada ya kuwa na muendelezo wa kuonekana wakiwa pamoja mara kwa mara kwenye viwanja mbali mbali vya kukulia bata.