
Mpenzi wa zamani wa msanii Weezdom, Mylee Stacy ametishia kumchukulia hatua kali za kisheria msanii huyo mara baada ya hivi majuzi kumporomeshea matusi mazito kwa madai ya kuingilia mahusiano yake mapya.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mylee Stacy amepost AOB ikionyesha namna ameandikisha taarifa katika kituo cha polisi cha Ruaka jijini Nairobi huku akisema kuwa ameamua kufungulia weezdom mashtaka kwa sababu amechoshwa na vituko vyake vya kumvunjia kila mara kwa kashfa za uongo ambazo kwa mujibu wake imeshushia brand na kumuathiri kiakili.
Mrembo huyo amekanusha madai yaliyoibuliwa na weezdom kuwa amekuwa akimtumia jumbe za mapenzi na kumpigia simu mke nyakati za usiku kwa kusema kuwa madai hayo ni ya uongo kwani ni njia weezdom kutafuta uhuruma kwa umma.
Hata hivyo mchumba mpya wa Weezdom, Carol Leehavi amekingia kifua msanii huyo a kwa kudai kuwa Mylee Stacy alimsaliti Weezdom kwa kutoka kimapenzi na wanaume mbali mbali jambo ambalo lilipelekea mahusiano yao kuvunjika.