
Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchini Uganda Exodus amewaomba radhi wafuasi wake na wakristo kwa tuhuma zilizomuandama kwa miaka mingi ikiwemo kunywa pombe.
Katika tamasha la “Katonda Wa Banaku akola” la Mchungaji Wilson Bugembe juzi kati, Exodus alijipata akiangua kilio huku akipiga magoti katikati ya performance yake na kusema kwamba anajutia makosa yote aliyoyafanya kipindi cha nyuma.
“Mambo mengi yanasemwa kunihusu. Wamesema nakunywa pombe. Wengine wanasema mimi ninapenda wanawake. Mambo mengi yanayosemwa si ya kweli, lakini yamenichafua. Lazima niombe msamaha kwa sababu watu wanawaamini,” alisema.
Msanii huyo amekiri pia kuna kipindi alikuwa anabugia pombe kupindukia lakini baada ya kupata wokovu aliacha.
“Sitakataa. Niliwahi kunywa pombe lakini niliacha. Pombe sio nzuri. Nilikuwa kijana, kwa sasa mimi ni mzee nafanya maamuzi bora,” alimalizia.
Mwaka wa 2019 wakati wa mahojiano na Just Comedy, hakukanusha madai ya kunywa pombe bali alinukuu kitabu cha Methali 23:20-23.
“Usiwe mmoja wa walevi wa divai,wala walafi wenye kupenda nyama, maana walevi na walafi wataishia kuwa maskini,anayetumia siku yake kusinzia atavaa matambara.”
Jibu lake liliibua hisia mseto miongoni mwa mashabiki zake lakini baadae alionekana kwenye moja ya picha akiwa na chupa ya Hennessey.