
Msanii wa muziki wa Hip Hop kutoka Tanzania, Fid Q amesema huwa hasikilizi nyimbo zake hasa pale anapokuwa anaandaa albamu ili kuepesha nyimbo kufanana.
Katika mahojiano na XXL ya Clouds FM Fid Q amesema “Kiukweli sina ngoma yangu katika playlist yangu, kwa ufupi sijisikilizi kabisa, na sijisikilizi kwa sababu sasa hivi nipo chimbo naandaa albamu ya nne”
“Kwa hiyo ninapokuwa naandaa albamu huwa sina tabia ya kujisikiliza kabisa kwa sababu ukijisikiliza ndio unakuta ngoma ina sound kama ile kule au hii imeingiliana baadhi ya vitu na ile kule,” amesema Fid Q
Kauli ya Fid Q inakuja mara baada ya hivi karibuni kutoa orodha ya nyimbo 20 anazozikilisha lakini hakukuwa na nyimbo yoyote toka kwake jambo liloacha maswali.
Utakumbuka Fid Q ameshaachia albamu tatu ambazo ni Vina Mwanzo Kati na Mwisho, Propaganda na KitaaOlojia