
Shirikisho la soka Duniani FIFA limetangaza kuwa dirisha dogo la usajili la mwezi januari 2025 limeweka rekodi ya matumizi makubwa ya pesa kwa ongezeko la asalimia 58 ukilinganisha na dirisha dogo la usajili lililopita la mwaka 2024.
FIFA imeweka wazi kuwa katika shughuli zote za usajili zilizofanywa na vilabu Duniani kote kwenye dirisha Dogo lla mwaka huu 2025 kiwango cha pesa kilichotumika ni pesa za marekani Dola Bilioni 2.35 ambayo ni zaidi ya Trilioni 6 kwa pesa ya Tanzania.
Takwimu za FIFA zimeonyesha jumla ya sajili 5,863 zimefanyika kwa njia rasmi za FIFA kwenye dirisha dogo kati ya Januari 1, 2025 hadi Februari 4, 2025. Ikiwa ni ongezeko la asilimia 19.1 ya rekodi ya awali ya idadai kubwa ya wachezaji waliosajiliwa kwenye dirisha dogo.