
Nyota wa muziki wa Dancehall Kutoka nchini Uganda Fik Fameica ameachia rasmi orodha ya ngoma zinazopatikana kwenye Album yake mpya inayokwenda kwa jina la “King Kong”
Fik Fameika amethibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuonesha tracklist hiyo yenye jumla ya mikwaju 14 ya moto.
Album hiyo imewakutanisha mastaa kama Eddy Kenzo, Geosteady, Bruce Melody, Vanessa Mdee na Mozelo Kids.
King Kong ambayo ni album ya kwanza kwa mtu mzima Fik Fameica inatarajiwa kuingia sokoni rasmi Ijumaa hii Oktoba 7 mwaka 2022.