Gossip

Fik Fameica Afunguka: Sitaki Mwanamke Aliyechubua Ngozi

Fik Fameica Afunguka: Sitaki Mwanamke Aliyechubua Ngozi

Rapa kutoka Uganda, Fik Fameica, amezua mjadala mitandaoni baada ya kufunguka kuhusu aina ya mwanamke anayependelea kuwa naye kwenye mahusiano ya kimapenzi. Msanii huyo, ambaye kwa sasa yuko single na hajawahi kutangaza hadharani uhusiano wowote, amesema ana matarajio ya kuwa na mpenzi mwenye sifa maalum.

Akizungumza na wanahabari kuelekea maandalizi ya tamasha lake linalotarajiwa kufanyika Septemba 5 mwaka huu katika uwanja wa Lugogo Cricket Oval, Fameica ameeleza kuwa angependa kuwa na mwanamke mwenye ngozi ya asili, hasa rangi ya kahawia au chocolate, na kwamba hana hamu ya kutoka na mwanamke aliyechubua ngozi.

Sanjari na hilo, rapa huyo amesisitiza kuwa anahitaji mwanamke mwenye akili na mchapa kazi, atakayechangia katika maendeleo yake ya kibinafsi badala ya kuishia tu kwenye mahusiano ya kawaida ya mapenzi.

Hata hivyo, Fik Fameica amebainisha kuwa kwa sasa hana haraka ya kuingia kwenye ndoa, kwani anataka kuelekeza nguvu na muda wake kwenye muziki pamoja na ukuaji wake binafsi.

Kauli zake zimepokelewa kwa hisia mseto mitandaoni, baadhi ya mashabiki wakionyesha kufurahishwa na uwazi wake huku wengine wakijadili vigezo alivyovitaja kuhusu mapenzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *