Sports

Fiorentina Yakubali Kumsajili Edin Dzeko Kutoka Fenerbahçe

Fiorentina Yakubali Kumsajili Edin Dzeko Kutoka Fenerbahçe

Klabu ya Fiorentina ya Serie A nchini Italia imekubali kumsajili mshambuliaji mkongwe Edin Dzeko kutoka Fenerbahçe ya Uturuki.

Dzeko mwenye umri wa miaka 39, anatarajiwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja utakaomuwezesha kubaki kwenye klabu hiyo hadi Juni 2027. Katika historia yake barani Ulaya, amewahi kucheza kwa vilabu kama Wolfsburg (2007-2010), Manchester City (2011-2015), AS Roma (2016-2021), na Inter Milan (2021-2023), kabla ya kuhamia Fenerbahçe ambapo amekuwa msimu huu.

Mchezaji huyu amefanikiwa kushinda mataji matano wakati akiwa Manchester City, ikiwemo mataji mawili ya Premier League, Kombe la FA, Kombe la Carabao, pamoja na Community Shield.

Usajili huu unalenga kuongeza uzoefu na ufanisi katika safu ya ushambuliaji ya Fiorentina msimu ujao.