
Ni Rasmi sasa mwanadada Fridah Kajala ni meneja wa Lebo ya Konde Music Worldwide.
Kajala ameongezeka kwenye uongozi wa Konde music ikiwa ni tamanio la Harmonize ambaye ndiye CEO wa lebo hiyo, kumtaka asimamie biashara yake ya Muziki.
Kajala ametangazwa rasmi na Choppa_ambaye ni mmoja wa mameneja wa Harmonize, kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika; “Allow Me To Welcome In Management Team New C.E.O And Manager Kajala Frida I’m Excited To Work With You Shem #kondegang4you“.
Naye Harmonize alishusha comment kwenye posti hiyo yenye maneno yanayosomeka; “Big Team, Big Dream” huku Kajala akiachia emoji za moto na kuonyoosha mikono juu.
Utakumbuka, Harmonize kabla hajarudiana na mpenzi wake Kajala, aliwahi kusema kwamba anatamani siku moja akirudiana na mrembo huyo, awe meneja wake.