Entertainment

Fully Focus akata kiu ya mashabiki zake na EP mpya “African Ambassador”

Fully Focus akata kiu ya mashabiki zake na EP mpya  “African Ambassador”

Hatimaye mwanamuziki mwenye asili ya Kenya anaishi nchini Marekani Fully Focus amekata kiu ya mashabiki zake na EP mpya inayokwenda kwa jina la African Ambassador.

EP hiyo ambayo ameitaja kuiandaa kwa takribani miaka minne imebeba jumla ya mikwaju 10 ya moto huku zote zikiwa ni kolabo.

Fully Focus amewashirikisha wasanii mbali mbali wa humu nchini na nje ya Kenya kama Fik Fameica, Sho Madjozi, Bien, Nyashinski na wengine kibao.

EP ya “African Ambassador” ni kazi ya kwanza kutoka kwa Fully Focus tangu aanze safari yake ya muziki.

Hata hivyo EP hiyo inapatikana ‘Exclusive’ kupitia mitandao yote ya kusikiliza na kuuza muziki duniani kama vile Apple Music na Spotify

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *