Entertainment

Geofrey Lutaaya Ataka Ambulance Aliyotoa Kwa Wananchi Irejeshwe Baada ya Kushindwa Ubunge

Geofrey Lutaaya Ataka Ambulance Aliyotoa Kwa Wananchi Irejeshwe Baada ya Kushindwa Ubunge

Mwanamuziki aliyegeukia siasa nchini Uganda Geofrey Lutaaya ameripotiwa kutaka ambulance aliyoinunua kwa wananchi wakati wa kampeni irejeshwe, kufuatia kushindwa kwake kwenye uchaguzi wa ubunge uliomalizika hivi karibuni.

Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu, Lutaaya ametoa makataa ya mwezi mmoja akitaka ambulance hiyo irudishwe kwake. Inadaiwa kuwa msanii huyo amechukizwa na matokeo ya uchaguzi baada ya kupoteza kiti cha ubunge, hali iliyomfanya abadili msimamo wake kuhusu msaada huo alioutoa kwa wananchi.

Wakati wa kampeni, Lutaaya alinunua ambulance ambayo aliikabidhi kwa jamii kama sehemu ya mchango wake katika kuboresha huduma za afya, hatua iliyopokelewa kwa furaha kubwa na wakazi wa eneo la Kakuuto.

Hata hivyo, hatua ya sasa ya kutaka irejeshwe imeibua maswali na hasira miongoni mwa wananchi, wengi wakisema msaada huo ulikuwa kwa manufaa ya umma na haukupaswa kuwa wa masharti ya kisiasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *