Entertainment

Gloria Bugie Ashinda Tuzo ya Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki

Gloria Bugie Ashinda Tuzo ya Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki

Nyota wa muziki anayechipukia kwa kasi kutoka nchini Uganda, Gloria Bugie, ameibuka mshindi wa tuzo ya Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki (Best Female Artist East Africa) katika kilele cha tuzo za Zikomo Africa Awards 2025.

Akizungumza kwa hisia kali mara baada ya kupokea tuzo hiyo jukwaani, Bugie hakuweza kuficha furaha yake, akitoa shukrani za dhati kwa Mwenyezi Mungu pamoja na mashabiki wake kwa kumuwezesha kufikia mafanikio hayo makubwa ndani ya kipindi kifupi cha safari yake ya muziki.

Tuzo hizo zilizofanyika usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam, zimeshuhudia Gloria Bugie akiweka historia baada ya kuwashinda wapinzani wakubwa na wenye majina mazito katika kiwanda cha muziki wa ukanda huu.

Katika kipengele hicho kilichokuwa na ushindani mkali, Bugie aliwabwaga wasanii wenye ushawishi mkubwa akiwemo Spice Diana (Uganda), Abigail Chams na Phina kutoka Tanzania, pamoja na Nikita Kering wa Kenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *