LifeStyle

Gloria Ntazola Ajivunia Maisha ya Mpango wa Kando, Asema Anaishi kwa Furaha

Gloria Ntazola Ajivunia Maisha ya Mpango wa Kando, Asema Anaishi kwa Furaha

Mrembo wa mitandaoni Gloria Ntazola ameendelea kuzua gumzo baada ya kufichua wazi kwamba yeye ni mmoja wa wanawake walio mipango ya kando. Kwa mujibu wa maelezo yake, hatua hiyo imemletea furaha na amani kwa sababu amekuwa akipata kila kitu anachohitaji kutoka kwa mwanaume wake.

Ntazola alifafanua kuwa mwanaume huyo amekuwa akimhudumia kikamilifu kwa kumpatia mahitaji ya msingi ikiwemo gari na matumizi ya kila siku. Anaeleza kuwa mara nyingi anapohisi hakupata anachotaka, humtishia mpenzi wake kwamba atamfichulia siri kwa mke wake, na ndipo hupokea alichokuwa akikitafuta.

Mrembo huyo ameshauri wanawake wakubali hali ya kuwa mipango ya kando badala ya kupigania nafasi ya wake wa kweli kwa wanaume wao.

Kwa mujibu wa kauli yake, Ntazola anasema wanaume wengi tayari wanatoka kimapenzi na wanawake zaidi ya mmoja, hivyo wanawake wasijisumbue kujipendekeza kuwa wao ndio wake halisi  ilhali ukweli ni kwamba uaminifu haupo.

Kauli hiyo imewasha mitandao kwa kasi, huku baadhi ya mashabiki wakimpongeza kwa ujasiri wa kusema ukweli wake, na wengine wakimshutumu vikali wakidai anahalalisha usaliti na kuvunja heshima ya ndoa.

Mjadala unaoendelea umeibua maswali kuhusu maadili ya mahusiano ya kisasa, wengi wakijiuliza iwapo kauli ya Ntazola ni taswira halisi ya uhusiano wa sasa au ni mbinu yake ya kutafuta kiki mtandaoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *