
Google imeweka uwezo wa simu kurekodi video katika wakati wa dharura kwenye Android 12. Imeweka uwezo wa kurekodi video automatic endapo mtu akibonyeza power button zaidi ya mara 5 au unapokwepo katika hali ya hatari.
Katika sehemu ya Emergency SOS, mtumiaji anaweza kuwasha option ya “Record emergency Video” ambapo endapo ukibonyeza Power Button mara 5 na kuendelea, moja kwa moja simu itakuwa katika SOS Mode, itakuwa inarekodi video huku ikipiga simu ya Emergency Services.
Video za dharura inaweza kuwa na urefu wa dakika 45 na ikubwa wa 10MB kwa dakika moja ili kusaidia storage na kufanya backup. Hii itasaidia mtu akipata matatizo, anaweza kutumia simu yake kurekodi ushahidi kwa Video.
Google imesema ukirekodi video, kama upo unatumia huduma ya internet; video hiyo inakuwa inajisevu ili endapo simu yako ikifa au kuibiwa ile video itabaki katika Cloud Storage yako.