Tech news

Google Yazindua Kipengele Kipya cha Recovery Contacts kwa Usalama wa Akaunti

Google Yazindua Kipengele Kipya cha Recovery Contacts kwa Usalama wa Akaunti

Google imeanzisha kipengele kipya kiitwacho Recovery Contacts, kinacholenga kusaidia watumiaji wa huduma zake kurejesha akaunti zao kwa urahisi zaidi endapo watakumbwa na changamoto kama kupoteza simu, kuibiwa, au kushindwa kutumia namba yao ya simu kupata PIN ya kuingia kwenye akaunti.

Kupitia huduma hii mpya, mtumiaji wa akaunti ya Google atakuwa na uwezo wa kuteua rafiki wa karibu au mwanafamilia anayeaminika kuwa kama mtu wa kusaidia katika urejeshaji wa akaunti (account recovery). Mtu huyu ataunganishwa kama “recovery contact”, na ataweza kusaidia mtumiaji kupokea PIN code ya muda ya kusaidia kuingia tena kwenye akaunti.

Ni muhimu kufahamu kuwa recovery contact hatakuwa na uwezo wa kuingia kwenye akaunti ya mtumiaji, wala kuona taarifa zozote za ndani ya akaunti hiyo. Jukumu lake litakuwa ni kupokea PIN kutoka Google pale itakapohitajika kusaidia katika mchakato wa urejeshaji.

Hatua hii inakuja kama sehemu ya jitihada za Google kuimarisha usalama wa akaunti za watumiaji na kuwasaidia wanaopoteza njia ya kawaida ya kuingia hasa kutokana na ongezeko la matukio ya wizi wa simu na changamoto za kiufundi zinazoweza kuziba njia ya kuingia kwenye akaunti.

Kwa sasa, huduma ya Recovery Contacts inapatikana kwa hatua za majaribio kwa watumiaji wa baadhi ya huduma za Google, na inatarajiwa kuenea kwa watumiaji wote duniani katika kipindi kifupi kijacho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *