Entertainment

Gravity Omutujju mbioni kuwekeza kwenye shughuli ya kuandaa matamasha ya muziki

Gravity Omutujju mbioni kuwekeza kwenye shughuli ya kuandaa matamasha ya muziki

Rapa Gravity Omutujju amedokeza mpango wa kuwekeza biashara ya kuwasimamia wasanii na kuandaa matamasha ya muziki.

Kwenye mahojiano yake hivi karibuni amesema amechukua hatua hiyo kwa  sababu mapromota wengi wamekuwa wakiingiza pesa nyingi kupitia matamasha ya muziki.

Hitmaker huyo wa “Enyama” amesema ana uwezo wa kufanya muziki sambamba na kuwasimamia kwa wakati mmoja bila changamoto yeyote.

“I’m going to start promoting musicians and organizing their events because I have seen there is money. I will take on a musician and have them perform here by January,” alisema kwenye mahojiano yake

Utakumbuka tamasha la Gravity Omutujju ambalo lilifanyika huko Cricket oval lugogo lilitayarisha na kampuni ya Balaam marketing and Promotions.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *