
Mwanamuziki wa nyimbo za injili nchini Guardian Angel ameachia rasmi album yake mpya inayokwenda kwa jina la Victory.
Victory imebeba jumla ya mikwaju 10 ya moto huku ikiwa na kolabo 3 pekee.
Guardian Angel ameshirikiana na wakali kama Solon Mkubwa,Goodluck Gozbert na Moji Short Baba
Album ya “Victory” ni album ya pili kwa mtu mzima guardian angel tangu aanze safari yake ya muziki baada ya Thanks for Coming iliyotoka mwezi mei mwaka huu ikiwa na jumla ya mikwaju 10 ya moto.
Hata hivyo Victory album inapatikana ‘Exclusive’ kupitia mitandao yote ya kukisikiliza na kuuza muziki duniani kama vile Boomplay,Spotify na Apple Music