LifeStyle

Guardian Angel Afunguka Kuhusu Shinikizo la Kupata Mtoto na Esther Musila

Guardian Angel Afunguka Kuhusu Shinikizo la Kupata Mtoto na Esther Musila

Mwanamuziki wa nyimbo za injili Guardian Angel ameweka wazi msimamo wake kufuatia shinikizo kutoka kwa baadhi ya mashabiki wanaomtaka yeye na mkewe Esther Musila kupata mtoto.

Akipiga stori na Plugtv, amesema hana wasiwasi kuhusu suala hilo, akifafanua kuwa uhusiano wao haukujengwa kwa msingi wa watoto bali kwa upendo wa dhati kati yao. Kwa mujibu wake, maagano yao yalitoa kipaumbele kwa upendo, na watoto ni kama nyongeza tu katika maisha yao.

Hitmaker huyo wa Kimya, ameongeza kuwa kama watapata mtoto, watamshukuru Mungu kwa baraka hiyo, na endapo hilo halitatokea bado wataendelea kufurahia maisha yao kwa amani na furaha.

Msanii huyo pia ameonyesha kutoridhishwa na shinikizo kutoka kwa watu wanaoingilia maisha yao ya kifamilia, akisema haelewi lengo la wale wanaowataka wapate mtoto kwa lazima.

Guardian Angel na Esther Musila wameendelea kudumisha ndoa yao kwa upendo mkubwa licha ya ukosoaji kutoka kwa baadhi ya watu mitandaoni. Wawili hao wameonyesha kwamba upendo wa dhati haupimwi kwa umri, watoto au matarajio ya watu bali kwa maelewano na kuheshimiana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *