
Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Kenya Guardian Angel ametoa changamoto kwa makanisa kuanza kuunga mkono kazi za wasanii wa nyimbo za injili nchini humo.
Kupitia ukurasa wa Instagram amesema wasanii wengi huenda wakaacha kujihusisha na muziki huo kabla mwaka 2023 haujaisha na kugeukia muziki wa kidunia kama hawatapata uungwaji mkono kutoka kwa wakristo.
Hata hivyo amesisitiza kuwa iwapo makanisa yataitikia wito huo hakuna msanii wa nyimbo za injili ataacha muziki huo kwa kuwa wengi wao wanatapitia mazingira magumu kwenye masuala ya kuingiza riziki kupitia muziki wao.
“2023 THE CHURCH MUST BEGIN TO SUPPORT KENYAN GOSPEL MUSICIANS…Otherwise things will be tough. Most of them might close down before the End of the Year:”
“Hakuna msanii wa GOSPEL ataacha gospel tena sababu anaimba akiteseka….Choose what to do with This information”, Aliandika.