Entertainment

GUARDIAN ANGEL AWAJIBU WANAODAI MUZIKI WA INJILI HAUNA PESA

GUARDIAN ANGEL AWAJIBU WANAODAI MUZIKI WA INJILI HAUNA PESA

Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Guardian Angel amewatolea uvivu wanaodai kuwa wasanii wa gospel wamefulia kiuchumi.

Katika mahojiano yake hivi karibuni Guardian Angel amesema madai ya kuwa muziki wa injili hauna pesa hayana ukweli wowote ambapo ameenda mbali zaidi na kusema kuwa yeye ni moja kati ya wasanii ambao wana mkwanja mrefu  na hata ikitokea ameacha muziki pesa zake zitamsaidia kujikimu kimaisha.

Katika hatua nyinngine amepinga madai kuwa Ringtone ameacha muziki wa injili kwa kusema kwamba haamini kabisa kama msanii huyo amekimbilia muziki wa kidunia kwani huenda anatumia jambo hilo kutengeneza mazingira ya kuzungumzia.

Guardian Angel ametoa kauli hiyo baada ya walimwengu kuhoji kuwa tasnia ya muziki nchini kenya haina pesa na ndio maana wasanii wengi waliokuwa wanafanya muziki huo wamegeukia muziki wa kidunia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *