Entertainment

HAMISA MOBETTO ALAMBA DILI NONO LA UBALOZI WA VIPODOZI VYA WHITENICIOUS

HAMISA MOBETTO ALAMBA DILI NONO LA UBALOZI WA VIPODOZI VYA WHITENICIOUS

Mwanamuziki na mwanamitindo kutoka Tanzania Hamisa Mobetto amelamba dili nono la ubalozi wa vipodozi vya White nicious kwa upande wa Bara la Afrika akimsaidia mwanadada Blac Chyna ambaye ni Balozi wa bidhaa hizo.

Mobetto ametangazwa rasmi Machi 2, mwaka wa 2022 kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa bidhaa hizo za asili zenye uwezo wa kupendezesha ngozi bila ya madhara.

Akithibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mobetto amesema vipodozi hivyo vya asili havina kemikali inayoharibu ngozi na kwamba vimethibitishwa na mamlaka husika kutumika kwa wanaume na wanawake. Lakini Pia ametaja bidhaa hizo ni kongwe sokoni zikiwa na miaka 30.

Hata hivyo inaonekana Milango ya kibiashara inazidi kufunguka kwa mwanamitindo huyo kwani ukiachilia mbali kuwa balozi wa bidhaa hizi za urembo za kimataifa pia ni balozi wa kinywaji cha kishua cha Belaire

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *