
Staa wa Muziki wa Bongofleva Harmonize Ametangaza jina Rasmi la Album yake ambayo itaingia sokoni mwezi ujao.
Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram Harmonize ameipa album hiyo jina la “Smoker Vision na ameweka wazi album hiyo itatoka mwezi Juni mwaka huu wa 2022
Boss huyo wa Konde Gang ambaye jana aliweka wazi kuja na brand yake ya Sigara, hii inaenda kuwa album yake ya tatu baada ya “Afro East iliyotoka mwaka 2020 na “High School” iliyotoka mwaka 2021.