
Staa wa Muziki Nchini Tanzania Harmonize ametangaza mabadiliko ya Ratiba ya Kufanyika kwa tamasha lake la Afro East Carnival kutoka siku tatu hadi siku mbili.
Kupitia ukurasa wa Instagram harmonize_amesema kwa sababu ambazo zipo nje ya uwezo wake sasa tamasha hilo litaanza Siku ya ijumaa na kumalizika Jumamosi wiki hii,nhaa sio Alhamisi kama ilivyotangazwa mwanzo.
“Tulitamani Sana ….!!!! Kuimba Nanyi Siku (3) Ila Kutokana Na Sababu Zilizo Nje Ya Uwezo Wetu Tumeridhiaa Kuipisha Siku Ya Alhamisi..Kuacha Shughuli Zaki Elimu Ziendele…. SO YESS LETS GO FRIDAY & SARTUDAY afro east carnival TABATA SHULE”.
Ukumbukwe tamasha la Afro East Carnival’ litafanyika Jijini Dar Es Salaam machi 4 mwaka huu. Kwa mujibu Harmonize, tamasha hilo litawakutanisha kwenye steji moja nyota wakubwa kwenye kiwanda cha muziki Afrika Mashariki.