
Promota wa show kutoka Nchini Nigeria Deejay Chii analalamika kuwa msanii wa Bongofleva Harmonize ameshindwa kufanya show nchini Canada baada ya kulipwa kiasi cha Kshs. millioni 1.2.
Kupitia video inayosambaa mtandaoni Deejay Chii anasema licha ya kuwa walishafanya makubaliano na Harmonize kiasi cha kumlipa pesa zote alizokuwa anahitaji, Hitmaker huyo wa “Leave Me Alone” ameingiwa na jeuri ya kutopokea simu zake mpaka muda huu.
Kwa mujibu wa promota huyo anasema kwamba tayari jambo hilo amelifikisha mikononi mwa polisi nchini Tanzania na linafanyiwa kazi.
Harmonize alitakiwa kutumbuiza kwenye miji mitatu nchini Canada kuanzia Oktoba 7 hadi Oktoba 10 , 2022.
Hata hivyo mpaka sasa Harmonize hajajibu chochote kuhusiana na tuhuma hizo ila ni jambo la kusubiriwa.