Entertainment

HARMONIZE ADAI MASHINDANO YA BONGO STAR SEARCH YALIMSHAWISHI KUFANYA MUZIKI

HARMONIZE ADAI MASHINDANO YA  BONGO STAR SEARCH YALIMSHAWISHI KUFANYA MUZIKI

Staa wa Muziki wa Bongofleva Harmonize Anasema kwamba Mashindano ya Bongo Star Search ndio yalimshawishi kuingia katika uimbaji.

Kupitia Instagram yake Harmonize ameandika mengi huku akimpa sifa Nyingi muanzilishi wa Mashindano hayo ya BSS madam rita na kusema kuwa amekuwa ni chanzo cha vijana wengi kuzifikia ndoto zao.

Kauli ya Harmonize imekuja baada ya kumpa heshima ‘Madam Rita’ mbele ya mashabiki kwenye tamasha la burudani la Serengeti Music Festival Februari 13 kwa kumpigia magoti kama njia moja wapo ya kutoa shukran zake kwa kumsaidia kujenga kipaji chake.

Ikumbukwe kuwa boss huyo wa Konde Gang ni miongoni mwa wanamuziki waliowahi kushiriki Bongo Star Search (BSS) miaka mingi nyuma na kukosolewa vikali kwa uimbaji wake kwa kuambiwa hajui kuimba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *