
Hitmaker wa “Outside”, Msanii Harmonize ameshukuru meneja wa Diamond Platnumz, Sallam SK kwa kumuweka kwenye orodha ya wasanii waliofanya vizuri mwaka 2022.
Kupitia insta story yake amemshukuru Sallam SK kwa kumtaja namba 10 katika list yake ambapo ameenda mbali zaidi na kujifananisha na mchezaji nyota Duniani, Lionel Messi ambaye huvaa jezi namba kumi mgongoni.
“Thank You Kipara no Mara Waa!!!!. 10. MESSI+”, Ameandika.
Siku ya jana Sallam SK alitoa list yake ya wasanii 10 wa Bongo Fleva waliofanya vizuri mwaka 2022, akiwapanga kuanzia nafasi ya 1 mpaka ya 10.