
Staa wa muziki wa Bongo Fleva Harmonize amevunja rekodi ya Video iliyotazamwa zaidi ndani ya muda mfupi iliyowekwa na kundi la wasanii kutoka South Korean ‘BTS’.
Hii ni baada ya Video ya wimbo mpya wa Harmonize na Ibraah, Mdomo imeipata views milioni 1 YouTube ndani ya sekude 21 tu!.
Hivi karibuni video ya Ibraah, Rara iliweza kupata views zaidi laki 6 ndani ya dakika tatu lakini ikachukua siku nne kufikisha views milioni 1 YouTube.
Ikumbukwe Mei mwaka 2021, bendi kutoka Korea Kusini, BTS ilivunja rekodi mara baada ya video ya wimbo wao, Butter kufikisha views milioni 108.2 ndani ya saa 24 na kuivunjilia mbali rekodi iliyokuwa inashikiliwa na Black Pink toka Korea ambao video yao, How You Like That’ M/V ya mwaka 2020 ilipata views milioni 86.3 ndani ya saa 24.