LifeStyle

Harmonize Asema A List Stars Ni Darasa la Maisha kwa Mabinti wa Gen Z

Harmonize Asema A List Stars Ni Darasa la Maisha kwa Mabinti wa Gen Z

Staa wa muziki wa Bongo Flava, Harmonize, ametoa ujumbe wa mafunzo kwa mabinti wa kizazi cha Gen Z baada ya kuguswa na maudhui ya reality show ya A List Stars inayotikisa kwa sasa mitandao ya kijamii.

Kupitia Insta Story yake, Harmonize amesema simulizi zinazotolewa ndani ya A List Stars ni darasa la wazi kwa vijana, hasa mabinti wa Gen Z, kwa kuwa zinaonesha uhalisia wa maisha ya mastaa wa Bongo Movie ikiwemo maamuzi magumu, maumivu ya nyuma na athari za chaguo walizofanya.

Kwa mujibu wa Harmonize, thamani ya reality show hiyo ipo kwenye ukweli wake, akisema wahusika aliamua kuweka wazi historia zao ili iwe funzo kwa kizazi kinachokuja.

Hitmaker huyo wa Leo, ameongeza kuwa ingawa yaliyopita ya wahusika hayawezi kubadilishwa, kuyajua kunamsaidia kijana kufanya kujitambua, kujithamini na kuelewa gharama na majukumu yanayoambatana na umaarufu.

A List Stars, ni Reality Show inayowaleta pamoja waigizaji wa Bongo Movie kusimulia maisha yao halisi nje ya mwanga wa umaarufu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *