Entertainment

Harmonize Atangaza Kolabo Mpya na Alikiba

Harmonize Atangaza Kolabo Mpya na Alikiba

Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Harmonize, ametangaza ujio wa kolabo yake na Alikiba, jambo lililowasisimua mashabiki wengi wa muziki Afrika Mashariki.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmonize amesema kuwa wimbo huo mpya unakuja hivi karibuni na ameuhakikishia umma kuwa utakuwa hit ya mwaka.

Hatua hii imeonekana kama ishara ya umoja mpya katika muziki wa Tanzania, kwani wawili hao kwa muda mrefu wamekuwa wakihusishwa na ushindani wa kimuziki.

Hadi sasa Harmonize hajaweka wazi jina la wimbo huo wala tarehe rasmi ya kutoka, lakini matarajio ni makubwa kwamba ujio huo utaweka rekodi mpya kwenye muziki wa Bongo Fleva.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *